The House of Favourite Newspapers

Omog Akubali Kuanza Kazi Na Niyonzima Dar

0
Kiungo mpya wa Simba, Haruna Niyonzima.

WAKATI kikosi cha Simba kinaendelea kujifua nchini Afrika Kusini kikijiandaa na msimu ujao wa 2017/18, kiungo mpya wa timu hiyo, Haruna Niyonzima ameomba kutokwenda nchini humo kujiunga na wenzake, badala yake yeye ataunganisha moja kwa moja Dar es Salaam.

 

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Simba ambazo Championi Ijumaa limezipata zimedai kuwa, Niyonzima amefikia hatua hiyo kutokana na kukabiliwa na matatizo ya kifamilia katika siku za hivi karibuni jambo ambalo limemsikitisha Kocha wa Simba, Joseph Omog ambaye alitamani kuwa naye katika kambi hiyo.

 

“Niyonzima ameomba kutoshiriki katika kambi yetu ya Afrika Kusini kutokana na kuwa na matatizo kidogo ya kifamilia ambayo anataka kutumia muda huu kuyaweka sawa.

“Kwa hiyo ataungana na timu hapa Dar es Salaam ambayo itarejea nchini kwa ajili ya Tamasha la Simba Day.

 

“Kwa hiyo, niwaombe tu wapenzi na mashabiki wa Simba wasiwe na wasiwasi lakini pia wajiandae kuja uwanjani kwa wingi siku hiyo ambapo tutamtambulisha rasmi kama mchezaji wetu pamoja na wachezaji wengine wote tuliowasajili msimu huu,” kilisema chanzo hicho cha habari.

 

Hata hivyo, kwa upande Omog alipoulizwa kuhusiana na suala hilo alisema: “Bado taarifa hizo hazijanifikia lakini kama itakuwa hivyo basi sina tatizo tutaungana naye huko.

Stori: Sweetbert Lukonge | Championi Ijumaa

Leave A Reply