Omog Aomba Wiki Mbili Mtibwa

BAADA ya kuanza vibaya Ligi Kuu Bara msimu huu, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar raia wa Cameroon, Joseph Omog ameomba apatiwe muda wa wiki mbili ili kukinoa upya kikosi hicho na kuweka mambo sawa ili wafanye vizuri.

Mtibwa Sugar tayari imecheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara ambapo ilianza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mbeya Kwanza, kabla ya kutoka suluhu na Prisons.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru, alisema: “Timu yetu imeanza vibaya, ni tofauti na mipango yetu tuliyopanga sisi kama timu, kutokana na hilo, kocha ameomba wiki mbili ili kurekebisha makosa yasijirudie katika michezo inayofuata.

“Hivyo tunatarajia kikosi chetu kitafanya vizuri zaidi katika michezo inayofuata ya ligi. Tunawaomba mashabiki wetu wasikate tamaa kwa hiyo michezo ya mwanzo kwani ligi ndio kwanza imeanza na sisi mipango yetu bado ipo palepale kuwa nafasi nne za juu katika msimamo wa ligi.”

HAWA ABOUBAKHARI, Dar


Toa comment