The House of Favourite Newspapers

Omog Aweka Ngumu Ndugu wa Tambwe Kutua Simba

0
Mshambuliaji wa timu ya Yanga, Amissi Tambwe.

SIMBA imeamua kufuta mpango wa kumleta nchini Kocha Mrundi, Niyongabo Amars raia wa Burundi sawa na Amissi Tambwe wa Yanga, baada ya bosi wa benchi la ufundi, Joseph Omog kuweka ngumu ujio wake.

Simba ilikuwa na mpango wa kumuongeza kikosini Amars aliyewahi kuinoa Telecom ya Djibouti ili awe kocha msaidizi akichukua nafasi ya Jackson Mayanja raia wa Uganda.

Chanzo kutoka ndani ya Simba kimeliambia Championi Jumamosi kuwa, dili la kumleta Amars limeshindikana kutokana na Omog kutomuhitaji kufanya naye kazi huku akimataka Mayanja aendelee na kazi.

“Yule kocha wa raia Burundi, Niyongabo Amars hatokuja tena kwani Omog ameweka ngumu akitaka aendelee kufanya kazi na Mayanja na anaamini atafanya naye vizuri msimu ujao,” kilisema chanzo hicho.

SAID ALLY | CHAMPIONI JUMAMOSI

Leave A Reply