The House of Favourite Newspapers

P.I.M.P. Yampeleka 50 Cent lupango!

0

50-Cent1Marekani

RAPA maarufu dunia kutoka lebo ya G-Unit, 50 Cent amekamatwa na Kikosi cha Uslama na kupelekwa lupango huko Saint Kitts katika Visiwa vya Caribbean nchini Marekani.

Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita, Juni 25 baada ya rapa huyo kutumia maneno ya matusi wakati akifanya shoo kwenye tamasha lililohudhuriwa na watu zaidi ya 40,000 Visiwani humo.

Taarifa zilizochapishwa na Jarida la TMZ kabla ya tukio hilo zilieleza kuhusu 50 Cent kuonywa na vyombo vya usalama nchini Marekani kutokana na tabia yake ya kutumia maneno yenye maudhi, matusi/kutukana ama udharirishashi hasa akiwa jukwaani au kwenye nyimbo zake hivyo akapigwa marufuku kufanya kitendo hicho.

Inasemekana kuwa 50 Cent alitumia maneno kama “motherf**kin’” wakati akiimba wimbo wake wa  P.I.M.P. kwenye tamasha hilo hali iliyopelekea vyombo vya usalama kumtia nguvuni kwa kukiuka masharti na onyo alilopewa siku za nyuma.

#50cent #PIMP #stkitts #stkittsmusicvestifle

A video posted by Samantha Stowe (@yayysamm) on

Leave A Reply