The House of Favourite Newspapers

Pablo Apangua Kikosi Simba SC

0

MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Crispin Ngushi amesema ataitumia timu hiyo kama daraja la kwenda kucheza soka la kulipwa nje.

Ngushi ni kati ya wachezaji wanne waliotambulishwa na Yanga mara baada ya kusajiliwa na timu hiyo katika usajili huu wa dirisha dogo.

 

Wachezaji wengine watatu waliosajiliwa na timu hiyo ni Salum Aboubakari ‘Sure Boy’, Denis Nkane na Aboutwalib Mshery.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ngushi alisema kuwa moja ya malengo yake aliyojiwekea ni siku moja kuichezea moja ya klabu kubwa nchini ambayo yametimia hivi sasa.

 

Ngushi alisema kuwa kwa kupitia Yanga atatangaza soka lake kupitia mashindano makubwa wa kimataifa ambayo timu hiyo inashiriki.

“Ninaamini ndoto zangu zitafanikiwa za kucheza soka la kulipwa nje ya nchi ni baada ya kufika hapa Yanga ambayo itashirikishi michuano ya kimataifa.

 

“Yanga itanitangaza zaidi kikubwa hivi sasa ninapambania kupata namba katika kikosi cha kwanza, hilo nitafanikiwa ninaamini uwezo wangu. Nitahakikisha ninatumia vyema kila nafasi nitakayoipata uwanjani.”

JOEL THOMAS, Dar es Salaam

Leave A Reply