The House of Favourite Newspapers

Pablo Atambulisha Mifumo Miwili Simba

0

 ILIKUWA juzi Ijumaa, ndiyo siku ambayo kocha mpya wa Simba raia wa Hispania, Pablo Franco alianza kazi rasmi ya kukinoa kikosi hicho baada ya kupewa mkataba wa miaka miwili akichukua mikobwa ya Mfaransa, Didier Gomes.

 

Pablo alifungua dimba kwenye uwanja wa mazoezi uliopo Boko, Dar ambapo kazi hiyo alianza saa 10:20 jioni, huku Spoti Xtra likimshuhudia akianza na kuweka mfumo.

 

Katika mazoezi hayo, alichomeka plastiki ndefu zenye muundo na mtu, kisha akazipanga nne nyuma, nne katikati na mbele akaziweka mbili, ambapo jicho la Spoti Xtra lilibaini kuwa hilo lilikuwa ni zoezi la mfumo wa 4-4-2.

Kwa maana hiyo, mfumo wake wa kwanza katika timu, ni kutumia walinzi wanne, viungo wanne na washambuliaji wawili.

 

Kisha baadaye akawa amebadilisha zile plastiki na kuweka tatu nyuma, tano katikakati na mbili mbele, hapo akawa ametengeneza mfumo wa 3-5-2 ambao unatumiwa na timu nyingi duniani, ikiwa walinzi watatu, viungo watano na washambuliaji wawili.

 

Kwenye mifumo yote hiyo, Pablo alionekana kumganda sana Jonas Mkude ili awe kiunganishi kwenye eneo la kiungo, huku Ousmane Pape, Hassan Dilunga wakipewa jukumu la kuzalisha mashambulizi.

 

Jimmyson Mwanuke na Yusuph Mhilu, walipewa jukumu la kufunga, huku Abdulswamad Kassim alikuwa anaongeza watu kwenye kiungo. Pascal Wawa jukumu lake lilikuwa ni kuzima mashambulizi na kupiga mipira mirefu kutoka eneo la ulinzi kwenda kwa Gadiel Michael ambaye alikuwa anamimina krosi kutokea upande wa kushoto.

 

Zoezi hilo lilimkuna sana Pablo na mara nyingi alionekana kupiga kelele za pongezi akisema safi au mara nyingine ‘Bravo’.

 

Wakati kikosi cha Simba kikiwa na wachezaji wachache huku baadhi yao wakiwa wameenda kwenye majukumu ya timu za taifa, walichanganyika na vijana wa U20 ambao kwa kiasi kikubwa walionekana kuwapa changamoto.Baada ya mazoezi hayo, Pablo alisikika akisema: “Siku ya kwanza imekuwa bora na nzuri sana, hongereni.

Leave A Reply