The House of Favourite Newspapers

Pacquiao Mbioni Kustaafu Ndondi

0

BINGWA wa zamani wa mkanda wa uzito wa kati wa WBA Welter Weight, Manny Pacquiao amesema kwa sasa inatosha kwa maana ya kutaka kuachana na mchezo huo alioutumikia kwa kipindi kirefu.

Kauli ya Pacquiao mwenye miaka 42 inakuja baada ya familia ya bondia huyo kumtaka astaafu haraka.

 

“Kazi yangu ya ndondi tayari imekwisha Imefanywa kwasababu nimekuwa kwenye ndondi kwa muda mrefu na familia yangu inasema kuwa inatosha” 

Kwa upande mwingine, Promota wa Pacquiao, Sean Gibbons amesema bondia wake bado haja staafu rasmi ila anatazamia kupata jibu kamili siku chache zijazo.

Pacquiao aliyetangaza nia ya kugombea Urais wa Ufilipino kwenye Uchaguzi mkuu wa mwaka 2022, kama atastaafu basi pambano lake dhidi ya Yordenis Ugas wa Cuba mwezi uliopita mwaka huu litakuwa la mwisho, ambapo Pacquiao alipigwa na kushindwa kuutetea mkanda wa WBO.

 

 

 

Leave A Reply