The House of Favourite Newspapers

Panya Road Bado ni Tishio Dar!

0

1.Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Simon Sirro akionga na wanahabari (hawapo pichani).Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro

Jiji la Dar viunga vyake bado linaendelea kukumbwa na matukio ya ajabuajabu likiwemo la watu kuporwa, kukatwa mapanga, kuchomwa visu na kunyanyaswa kijinsia.

Katika ripoti kamili wiki hii, uchunguzi wa Wikienda umeangazia matukio hayo, mengi yakifanywa na vikundi vya vijana wadogo wanaojiita Panya Road ambao huanza kwa kujifunza karate mitaani.

Vijana hao ni wenye umri mdogo wa kuanzia miaka 18 na kuendelea ambao wengi wao huwa wanakimbia kwenda shule ambao ni wengi katika mitaa mbalimbali ya jijini Dar.

Baadhi ya maeneo korofi ya Panya Road ni pamoja na Mwanan-yamala, Tandale, Kijitonyama, Kawe, Kunduchi-Beach, Kibamba, Msakuzi, Tabata, Buguruni, Kigogo, Temeke, Mbagala-Chamazi na Mbande.

Katika ripoti hii, Wikienda lilifanya mahojiano na baadhi ya wakazi wa maeneo tajwa na wao kutoa mtazamo wao kuhusu janga la Panya Road.

MWANAISHA HAMIS WA BUGURUNI:

“Panya Road ni kundi hatari sana. Kinachoniuma mimi ni vijana wa umri mdogo ndiyo wengi kwenye hilo kundi, napata wakati mgumu sana kuona kizazi cha sasa kinavyoteketea.”

REHEMA WA KAWE:

“Niliwahi kuwashuhudia wakifanya uhalifu mtaani, kiukweli Panya Road huwa hakuna amani kabisa, kwani wanakuwa na mapanga, visu, mikuki, mishale na vitu vingine vyenye ncha kali.”

JAMES KIMARO WA TABATA:

“Nimewahi kushuhudia mtu mmoja akiwa amechomwa kisu na Panya Road. Kinachonishangaza ni intelijensia ya polisi kushindwa kuumaliza huo mtandao wa hao watoto hii ni aibu kubwa sana kwa jeshi hilo.”

MZEE JUMANNE WA TANDALE:

“Vijana wa sasa wanaharibikiwa na makundi ya ajabuajabu, unga, bangi na haya makundi ya kujifunza karate ndiyo yanayotusumbua mitaani. Namuomba Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ atumbue jipu la Panya Road wanatukosesha amani.”

RAHEL SADICK WA SINZA:

“Sina hamu na Panya Road wala sitaki hata kuwasikia kwani walishawahi kunipora mkoba, simu na fedha, walinipiga sana, hawafai na wanatakiwa kufanyiwa kazi kikamilifu.”

AYOUB MWANANDA WA SEGEREA:

“Ukiangalia kinachosa-babisha vijana hao kufanya uhalifu, ni ugumu wa maisha lakini naamini ingekuwa ni vizuri kama umoja huo walionao wakautumia kwa kuomba kazi, maeneo kwa ajili ya kilimo, ufugaji na mambo ya maana na siyo kufanya uhalifu.”

SAKINA JOHN WA KUNDUCHI:

“Bila shaka serikali ina nguvu na mkono mrefu ila inashangaza kuona kuwa kikundi kidogo, tena cha watoto kinasumbua na kuwakosesha amani wananchi, hii haikubaliki. “Tunashuhudia kila siku mafisadi wakitumbuliwa, sasa kwa nini Panya Road wasitumbuliwe?

“Makundi haya ya kihalifu yamekuwa ni tishio kwa watu wengi ambao wamekuwa wakipata mathara mbalimbali kutokana na makundi hayo. Ni wajibu wa serikali kulivalia njuga suala hilo ili kuwafanya wananchi na mali zao kusihi kwa amani.”

KAMANDA SIRRO ANASEMAJE?

Kwa upande wake, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro ameapa kupambana na makundi yote ya uhalifu na siyo Panya Road tu kwani kuna makundi mengine ya Hapa Kazi Tu, Mbwa Mwitu na Watoto wa Mbwa.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE:@shigongotz

Leave A Reply