The House of Favourite Newspapers

Paramagamba: Watetezi wa Haki za Binadamu ni Walezi wa Jamii

0
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Paramagamba Kabudi akisoma hotuba yake kwa niaba ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa,(wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na mwanamama aliyepata tuzo ya ngao kwa mchango wake.

 

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadanu na Utawala Bora (THBUB), Bahame Nyanduga, akiwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya wageni mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo.

WAZIRI wa Katiba na Sheria Prof. Paramagamba Kabudi amesema watetezi wa haki za binadamu ni watu muhimu  kote duniani kutokana na  kuwa walezi katika jamii yenye usawa na inayotambua na kuheshimu haki za binadamu.

Hayo aliyasema leo jijini Dar es Salaam kwenye maadhimisho ya nne ya Siku ya Watetezi wa Haki za Binadamu wakati alipomwakilisha aliyetakiwa kuwa mgeni rasmi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samiah Suluhu.

Akisoma hotuba yake kwenye hafla hiyo, alisema watetezi wa haki za binadamu wamekuwa wakijitolea kufanya kazi bila kuchoka katika kuhakikisha watu wanapata haki zao bila vikwazo vyovyote.

“Kufuatia majukumu mliyonayo katika nchi yetu kama watetezi wa haki za binadamu, serikali inatambua kazi zenu na inapobidi inafanya kazi na AZAKI ili kuhakikisha kuwa wananchi wanafurahia haki zao.

“Tumekuwa tukizingatia mawazo mengi muhumu na ushauri kutoka asasi za kiraia na watetezi wa haki za binadamu kwa ujumla.  Mfano mzuri ni kutungwa kwa sheria maalum ya makosa ya kujamiiana ya mwaka 1998 ambayo iliichangiwa kwa kiasi kikubwa na watetezi wa haki za binadamu hasa watetezi wa jinsia ya kike.

“Nimeskia kwamba tukio hili la leo limebeba  kaulimbiu maalum ambayo ni ‘Kuimarisha uhusiano kati ya watetezi wa haki za binadamu na serikali’. Hakuna shaka yoyote kuwa utekelezaji wa haki za binadamu katika nchi yoyote hutegemea sana wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na asasi za kiraia na umma kwa ujumla,” alisema.

Naye mwenyekiti wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (Tanzania Humuan Rights Defenders Coalition  – THRDC), Onesmo Olenguruwa,  alisema kuwa lengo kubwa la mtandao wa watetezi wa haki za binadamu nchini  ni kuweka na kuimarisha usalama na ulinzi  wa watetezi wa haki za binadamu nchini kote.

Alisema pia  kuimarisha ufanyaji kazi na asasi za kikanda na za kimataifa za kulinda na kukuza haki na majukumu ya watetezi wa haki za binadam huchangaia katika kuweka mazingira salama ya kazi kwa watetezi wa haki za binadamu.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply