The House of Favourite Newspapers

Paula, Kajala Kama Mapacha Vile

0

PAULA Kajala; ni modo maarufu kwenye mitandao ya kijamii ambaye ni mtoto wa prodyuza P Funk Majani na mwigizaji mkubwa wa Bongo Movies, Kajala Masanja au Mama Pau.

 

Paula ambaye yupo masomoni nchini Uturuki amekuwa maarufu zaidi baada ya kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na staa wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa almaarufu Rayvanny akidaiwa kumpora kwa Fahyma.

 

Paula ameposti picha akiwa na mama yake (Kajala) wakiwa wamevaa nguo sare na kuandika; “Kama mapacha vile, kumbe mtoto na mama yake, asante mama kwa kunilandisha nakupenda…”

 

Paula anamaanisha kwamba anafanana mno na mama yake, Kajala kiasi kwamba mtu anaweza akawachanganya akijua ni mapacha kumbe ni mtoto na mama yake. Hata hivyo, Paula anamkubali na kumpenda mno mama yake ambaye amekuwa naye bega kwa bega hivyo anaahidi kumpenda milele.

Stori; Imelda Mtema, Dar

Leave A Reply