The House of Favourite Newspapers

Paula na Jux Mambo ni Moto Wadaiwa Kuwa Wapenzi, Rayvanny Anuna!

0
Staa wa muziki wa RnB Bongo, Juma Jux.

Paula Kajala; ni mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii (sosholaiti) nchini Tanzania ambaye kwa muda sasa amekuwa akihusishwa kutoka kimapenzi na staa wa muziki wa RnB Bongo, Juma Jux.

 

Madai ya penzi la Paula na Jux yalidaiwa kusababisha aliyekuwa mpenzi wa mrembo huyo, Rayvanny na Jux kutokuelewana kiasi cha kublokiana na hata kwenye Instagram zao tayari Rayvanny kamu-unfollow Jux na hata Jux pia kamu-unfollow Rayvanny.

 

Madai hayo yamekuwa ya moto mno baada ya mrembo huyo kusema kwamba, aachwe amng’ang’anie mpenzi wake kwa sababu anamdekeza.

“Acheni nimng’ang’anie, ananidekeza…” Alisema Paula.

 

Baada ya Paula kusema hivyo ndipo baadhi ya watu wakaibuka na madai kuwa, anayemdekeza si mwingine bali ni Jux.

Mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii (sosholaiti), Paula Kajala.

Hata hivyo madai ya Paula kutoka kimapenzi na Jux hayajawahi kuthibitishwa popote na yeyote kati yao na wala hakujawahi kuwepo kwa video au picha yao ya pamoja bali kumekuwa na tetesi tu ambazo hazina ushahidi zaidi ya minong’ono ya watu wao wa karibu.

 

Taarifa ikufikie kwamba, ishu hiyo imemfika shingoni Paula na kujikuta akitokwa povu zito.

“Ifike mahali niheshimiwe, siyo kila mwanaume mnanihusisha naye, mtu sijawahi kusema hata kama nipo naye kwenye mahusiano, kila kukicha kunigonganisha naye, mara leo huyu, kesho huyu, hebu punguzeni shobo…” Amesema Paula akionesha kukerwa na ishu hiyo.

 

Baadhi ya watu wa karibu wanadai kuwa, huo ni mkwara tu kwani kuna watu wanajua mchezo mzima kuhusu Paula kwenda nyumbani kwa Jux wakisisitiza wanatoka.

 

Kwa upande wake, Jux hajawahi kusema chochote juu ya ishu hiyo tangu imeanza kuzungumzwa.

Kuna wakati walipiga picha sehemu moja nchini Afrika Kusini, lakini haikuwa picha ya pamoja isipokuwa ni ‘lokesheni’ tu zilifanana.

 

Stori za Paula na Jux ziliibuka baada ya mrembo huyo kutengana na msanii mwingine wa Bongo Fleva, Rayvanny ambaye sasa amerudi kwa mzazi mwenzake, Fahyma wanamlea mtoto wao, Jaydanny.

STORI NA SIFAEL PAUL | GPL

AHMEDY ALLY ANAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI…

Leave A Reply