The House of Favourite Newspapers

PEMBA: OFISI ZA CUF ‘ZABADILISHWA’ KUWA ZA ACT-WAZALENDO

TASWIRA katika Chama cha Wananchi (CUF) inazidi kunoga! Hivi ndivyo unavyoweza kusema kufuatia baadhi ya ofisi za chama hicho Zanzibar kuanza kubadilishwa rangi na kupakwa mwonekano wa rangi inayotumiwa na Chama cha ACT-Wazalendo.

 

Katibu wa CUF Wilaya ya Chakechake, Kusini Pemba, Saleh Nassor Juma, amesema wamepokea maagizo hayo kutoka ngazi za juu yakiwataka kuanza kubadili rangi za matawi ya chama hicho ambapo wameanza utekelezaji katika ofisi ya Jimbo la Chakechake.

 

Saleh ambaye yupo upande wa aliyekuwa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kwa vile wana mtaji wa watu hawawezi kuhuzunishwa na uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kumhalalisha Profesa Ibrahim Lipumba kuwa Mwenyekiti wa CUF badala yake wataendelea kutumikia chama kingine ambacho wataelekezwa hapo baadaye.

 

Katibu wa Jumuiya ya Vijana CUF, Khalifa Abdallah,  amesema wanajivunia umma walionao ambao unamuunga mkono Maalim Seif.  Vilevile, kiongoziwa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, alipohojiwa kuhusu suala hilo, alilizungumzia kwa ufupi:

“Ninachojua harakati za kudai demokrasia lazima ziendelee… Sisi tutamuunga mkono Maalim kwa hatua yoyote atakayochukua, kama kuna jambo Watanzania watajulishwa rasmi,” amesma Zitto.

Comments are closed.