The House of Favourite Newspapers

Perez: Kama Mbappe Anataka Kuja Real Madrid Basi Akubali Masharti Yetu

0
Nyota wa Timu ya Taifa ya Ufaransa na Klabu ya Paris Saint Germain, Kylian Mbappe

RAIS wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez ameibuka na kusema kuwa kama nyota wa Paris Saint Germain na Timu ya Taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe ana ndoto za kujiunga na klabu ya Real Madrid basi inamlazimu akubali masharti yahusuyo masuala ya masoko pamoja na haki za matangazo.

 

Perez ameyasema hayo huku kukiwa na fununua za nyota huyo kutokuwa na furaha ndani ya kikosi cha Paris Saint Germain licha ya kuwa amesaini mkataba mpya hivi karibuni.

 

Ikumbukwe Mbappe ni shabiki mkubwa wa Real Madrid na alishawahi kuweka wazi nia yake ya siku moja kucheza katika dimba la Santiago Bernabeu.

Rais wa Klabu ya Real Madrid, Florentino Perez

Aidha Perez amebainisha kuwa mbali za masuala ya masoko pamoja na haki za matangazo Mbappe anatakiwa pia kupunguza mshahara ili kuendana na viwango vya mishahara vinavyolipwa na klabu hiyo kwani asitegemee kama anaweza kupata mshahara kama anaoupata kwa sasa Pac de Princes.

 

Kwasasa Mbappe yupo na kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa katika mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia zinazofanyika nchini Qatar ambapo timu yake imefanikiwa kutinga katika hatua ya 16 bora ya mashindano hayo.

Leave A Reply