The House of Favourite Newspapers

Pichaz + Video: Arsenal Mabingwa wa FA Cup Baada ya Kuifunga Chelsea 2-1

0

Baada ya kusubiriwa kwa hamu mchezo wa fainali ya FA Cup kati ya Arsenal dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Wembley, hatimae May 27 2017 mchezo huo ambao ulikuwa unatajwa kama ndio utaamua hatma ya kocha Arsene Wenger ndani ya Arsenal ulichezwa rasmi.

Licha ya Arsenal hivi karibuni wamekuwa wakionekana hawafanyi vizuri, wamefanikiwa kuchukua taji lao la 13 la FA jana na kuwa club inayoongoza England kutwaa taji hilo mara nyingi zaidi ikifuatiwa na Man United waliyowahi kutwaa taji hilo mara 12.

Arsenal imefanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-1 magoli ambayo yalifungwa na Alex Sanchez dakika ya 4 na Aroon Ramsey dakika ya 79 ikiwa ni dakika 3 zimepita toka Diego Costa aifungie Chelsea goli la kwanza, ushindi sasa unamuwekea rekodi Arsene Wenger wa kuwa kocha pekee aliyewahi kutwaa mataji 7 ya FA katika historia ya Kombe hilo.

 

 

Leave A Reply