The House of Favourite Newspapers

Pikipiki, Televisheni, Simu Kukabidhiwa Leo, Tukio Zima Kurushwa Global TV Online -Live

Stori: GABRIEL NG’OSHA | UWAZI

WATU wanne walioshinda katika droo ndogo ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba iliyofanyika Februari 8, mwaka huu, leo Feb. 21, 2017 wataweka rekodi ya kuwa wa kwanza watakapokabidhiwa zawadi zao katika ofisi za Global Publishers, zilizopo Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Washindi hao ni Andrew Mtunguja wa Muheza Tanga aliyejishindia pikipiki, Amarosi Mgonja wa Mang’ula mkoani Morogoro aliyejishindia televisheni, Evans Stanley wa Kunduchi na Said Mohamed wa Kimara Dar ambao wote wamejishindia simu za kisasa (smartphones) na Gasto Peter wa Kimara pia aliyejishindia Dinner Set (vyombo vya jikoni).

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho alisema jana kuwa zoezi la kuchezesha droo ndogo litaendelea na kwamba washindi watazawadiwa kadiri watakavyopata. “Niwasisitize tu wasomaji wa magazeti yetu kuendelea kujaza kuponi na kuzituma kwetu kupitia anuani zilizopo kwenye kuponi au wapeleke kwa mawakala wetu walio nchi nzima au kwa wale wa Dar, wanaweza kuja moja kwa moja ofisini kwetu na kutuletea kuponi zao,” alisema.

Alisema katika msimu huu wa Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili, idadi ya zawadi pia zimeongezwa tofauti na mwaka jana, kwani kwa sasa kila mwezi watakuwa wakichezesha droo ndogo na zawadi kubwa ya pikipiki kutolewa, sambamba na zawadi zingine ndogondogo wakati wakielekea kumpata mshindi wa nyumba mwishoni mwa shindano.

 

Katika Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Kwanza, mshindi wa kwanza alikuwa ni Nelly Mwangosi kutoka mkoani Iringa ambaye ni mjasiriamali aliyeweza kupewa mjengo huo wenye thamani ya mamilioni ya shilingi uliojengwa Salasala, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Tukio lote litakuwa likirushwa moja kwa moja kupitia Global TV Online, kuanzia saa 5:00 asubuhi hii… SUBSCRIBE sasa usipitwe na matukio matukio yote nchini.

Comments are closed.