The House of Favourite Newspapers

Pingamizi la Sugu Lakataliwa Mahakamani, Arudishwa Rumande

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi jijini Mbeya imetupilia mbali pingamizi la upande wa utetezi la kutaka kutosikilizwa kwa ushahidi wa sauti katika kesi inayomkabili Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi  na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanual Masonga na kuamuru ushahidi huo usikilizwe mahakamani hapo.

 

Mahakamani imefikia uamuzi huo leo baada ya mvutano uliotokea jana Jumanne ambapo upande wa utetezi ukiongozwa na mawakili Boniface Mwabukusi na Hekima Mwasipu kuiomba mahakama kutopokea ushahidi huo kwa madai kuwa  una mapungufu ya kisheria.

 

Baada ya mahakama kukubali utetezi huo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Michael Mteite, shahidi namba tano katika kesi hiyo upande wa mashtaka Inspekta Joram Magova alitoa ushahidi wa sauti aliyowarekodi Sugu na Masonga kwa kufunga vipaza sauti ili kusikika kwa ufasaha mahakamani.

 

Sugu na mwenzake wanakabiliwa kwa makosa ya kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli, mnamo Desemba 30,2017 katika mkutano wa hadhara walioufanya kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge.

 

Kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo, askari waliimarisha ulinzi, huku wakiwazuia wafuasi wa Chadema kuingia katika jengo la Mahakama kusikiliza kesi hiyo licha ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Mwakagenda kuingia katika ukumbi wa Mahakama kufuatilia shauri hilo.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi kesho saa 4 asubuhi ambapo upande wa walalamikiwa utaanza kutoa utetezi baada ya leo upande wa mashtaka kukamilisha ushahidi wake.

Nabii Tito Mbaroni, Abainika na Ugonjwa wa Akili

Comments are closed.