The House of Favourite Newspapers

Pogba Aipeleka Man United Robo Fainali Europa

0

PAUL Pogba wa Manchester United na mshikaji wake Zlatan Ibrahimovic walitambulishwa wakitokea benchi kwenye mchezo wa Europa League ambao ulikuwa wa marudio.

 

Ibrahimovic wa AC Milan naye alibeba matumaini ya kufunga ila bahati haikuwa yake, Pogba mwenye miaka 28 alikuwa shujaa kwa kuwa alifunga bao la ushindi na kufanya ubao usome AC Milan 0-1 Manchester United.

 

 

Bao la Pogba dakika ya 48 linaipa nafasi United kusonga mbele hatua robo fainali kwa jumla ya mabao 2-1 kwa kuwa mchezo wa kwanza walitoka sare ya kufungana bao 1-1 ndani ya Old Trafford na wameshinda San Siro.

 

 

Pogba amerejea kwa kasi ndani ya uwanja kwa kuwa alikuwa akitibu majeraha tangu Februari 6, Ole Gunnar Solskjaer Kocha Mkuu wa United amesema kuwa ni furaha kwa timu pamoja na mashabiki kiujumla.

 

 

“Kupata ushindi na kusonga mbele kwetu ni furaha na ninawapongeza wachezaji kwa kuwa wamepambana kutafuta matokeo,” .

Leave A Reply