The House of Favourite Newspapers

Polisi Mbeya Wataja Chanzo Vifo Vya Watu Wawili Ruaha -Video

0

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Urlich Matei amesema uchunguzi wa kidaktari wa miili ya watu wawili pamoja na kichwa cha binadamu vilivyokutwa ndani ya hifadhi ya ruaha, umebaini kuwa chanzo cha vifo hivyo ni watu hao kushambuliwa na wanyama wakali wakiwemoviboko na mamba ndani ya hifadhi hiyo.

 

Kamanda Matei amesema hayo leo Aprili 28, 2021 na kuongeza kuwa miili hiyo iliyopatikana katika Vitongoji vya Magwalasi na Ikanutwa, Mbarali mkoani Mbeya, imetambulika kuwa ni ya wafugaji wawili, Salu Masanja na Ngusa Salawi pamoja na mvuvi mmoja, William Estobel.

Ameongeza kwa kuwataka wananchi hususan wafugaji, kuacha kuingia katika maeneo ya hifadhi kutokana na kuwepo kwa wanyama wakali kama viboko na mamba na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari hasa katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha mafuriko.

Leave A Reply