The House of Favourite Newspapers

Polisi Nchini Kenya Wamhoji Mchungaji Ezekiel Odero, Wafunga Kanisa lake

0

Polisi nchini Kenya wamemhoji mhubiri Ezekiel Odero na kufunga kanisa lake kuu la Mavueni ambalo lipo katika kaunti ya pwani ya Kilifi .

Mratibu wa eneo la Pwani Rhoda Onyancha alithibitisha kuwa mhubiri huyo alikuwa akihojiwa na polisi mjini Mombasa.

Onyancha amesema kamati ya usalama yae eneo hilo imeamua kumkamata mhubiri huyo wa kanisa la New Life Prayer Centre ili kumhoji kuhusu mafundisho yanayotolewa na kanisa lake .

Ameongeza kuwa watatoa taarifa zaidi kuhusu uchunguzi wao. Amesema kuwa watu waliokuwa katika kanisa hilo wameodolewa .

Kukamatwa kwa mhubiri huyo kumejiri baada ya kisa cha kupatikana kwa makaburi ya watu katika msitu wa Shakahola ambapo zaidi ya watu 90 wamethibitishwa kufa .Mhubiri mwingine Paul Mackenzie yuko rumande kuhusiana na tukio hilo .

WABUNGE WACHACHAMAA, WAIBANA SERIKALI KWA MASWALI MAZITO, MANAIBU WAZIRI WAJIBU | DODOMA

Leave A Reply