The House of Favourite Newspapers

Polisi Watuhumiwa Kumuua Mtoto wa Miaka 13

0

POLISI nchini Uganda, linachunguza mauaji ya Ester Naula(13) ambaye amedaiwa kupigwa risasi na polisi kwa kukutwa nje saa moja na robo usiku ambao ni muda wa kuwa ndani ikiwa ni sheria mpya za kujikinga na virusi vya ugonjwa wa corona.

 

Tukio hilo limetokea katika Wilaya ya Butaleja, Ester alikuwa ametoka kununua chapati, ambapo polisi alirusha risasi baada ya Ester na wananchi wengine kukimbia ili kuepuka kukamtwa.

 

Msemaji wa Polisi wa Mkoa wa Kusini, Moses Mugwe amethibitisha tukio hilo lililoacha majeruhi kadhaa na kwamba polisi aliyefanya tukio hilo ameshakamatwa.

 

Leave A Reply