The House of Favourite Newspapers

Prince Dube, Tigere Waikosa Simba

0

NYOTA watatu wa Azam FC, Prince Dube, Never Tigere na Bruce Kangwa, huenda wakaukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba utakaochezwa wikiendi hii kutokana na kuwa na majukumu kwenye timu yao ya taifa ya Zimbabwe.


Wazimbabwe hao tayari
wameungana na wenzao katika kambi ya kujiandaa na michuano ya AFCON
inayotarajiwa kuanza Januari 9
hadi Februari 6, mwakani nchini Cameroon.


Hivi karibuni, nyota hao ambao wanacheza kikosi cha kwanza cha Azam FC, wamejumuishwa kwenye kikosi cha awali cha Zimbabwe kabla ya kufanyika mchujo kesho Jumatano kupata kikosi ambacho kitashiriki AFCON.


Akizungumza na
Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria, amesema: “Tigere, Kangwa na Dube
wameitwa katika timu ya taifa
ya Zimbabwe kwa kambi ya muda kuchuja wachezaji watakaokwenda AFCON.

 


“Mchujo wao utafanyika
Desemba 29, kama watafanikiwa kupenya, watasalia hukohuko, lakini wakishindwa, watarudi haraka kuuwahi mchezo dhidi ya Simba.”

LIVE: MORRISON Amtibua PABLO, HITIMANA OUT SIMBA, MSHAHARA wa KIPA YANGA KUFURU | KROSI DONGO….

Leave A Reply