The House of Favourite Newspapers

Prisons vs Yanga SC… Rekodi Zinawatisha

0

KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze, amekiri kuwa mchezo wao wa leo dhidi ya Prisons utakuwa mgumu, hasa kutokana na rekodi nzuri ya wapinzani wao wanapocheza katika uwanja wa nyumbani wa Nelson Mandela uliopo Sumbawanga mkoani Rukwa.

Mara ya mwisho timu hizo kukutana ilikuwa katika mchezo wa raundi ya kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara msimu huu uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

 

Kaze ameliambia Spoti Xtra, kuwa ameweka mpango kazi wa kuhakikisha anaufungua ukuta wa Prisons na kupata matokeo mbele yao licha ya wapinzani wake kuwa wagumu.

 

“Kitu kizuri ni kwamba tumepata muda mzuri wa kujiandaa na mazoezi, na mazoezi ni mazuri na wachezaji wana nia ya kutafuta ushindi kwenye mechi hii na Prisons.“Prisons wana timu nzuri, wanajua kuzuia, wana mwalimu mwenye uzoefu wa ligi lakini na sisi tumejiandaa kulingana na uzito wa mechi, hii.

 

“Hakuna timu nyingi ambazo zimewafunga wakiwa hapa hivyo tunafahamu tunatakiwa kupandisha pafomansi kwa ajili ya kupata matokeo mazuri,” aliweka nukta Kaze.

Meneja wa Prisons, Prosper Mtevu, alizungumzia mchezo huo akisema:

“Tunaijua vizuri Yanga, mchezo wa raundi ya kwanza baina yetu tulipata matokeo ya sare, na wanaonekana kuwa na rekodi nzuri, lakini huwezi kushinda kila siku, hivyo inawezekana kabisa sisi tukaifanya ipoteze mchezo wake wa kwanza.”

STORI: JOEL THOMAS NA SAID ALLY, Dar es Salaam

Leave A Reply