The House of Favourite Newspapers

Makonda Kusakwa

0

MWANAHABARI mkongwe nchini Tanzania, Saed Kubenea, anakusudia kuiomba Mahakama ya Kinondoni, itoe wito mpya kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ili ahudhurie katika kesi aliyoifungua dhidi yake na Serikali. 

 

Taarifa hiyo imetolewa leo Alhamisi, tarehe 3 Februari 2022 na Wakili wa Kubenea, Hekima Mwasipu, akizungumza na wanahabari mahakamani hapo, baada ya kesi hiyo namba 1/2022, kuahirishwa hadi Jumanne ya tarehe 8 Februari mkwaka huu.

 

Katika kesi hiyo, Kubenea anaomba kibali cha mahakama kumshtaki Makonda, akidai Serikali kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) na Mkurugenzi wa Makosa ya Upelelezi nchini (DCI).

 

Imeshindwa kutekeleza majukumu yake ya kumshtaki kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka yanayomkabili. Katika kesi hiyo, Kubenea anaishtaki Ofisi ya DPP, DCI na Makonda.

 

Wakili Mwasipu amedai kuwa, ombi hilo wataliwasilisha mahakamani hapo Jumanne ijayo, wakati kesi hiyo ikienda kutajwa mbele ya Hakimu Aron Lyamuya. Amedai wanakusudia kuchukua hatua hiyo, baada ya jitihada zao za kumpata Makonda kugonga mwamba.

 

“Ni kweli kesi ilkuwa inakuja kwa ajili ya kutajwa lakini imeahirishwa hadi Jumanne na mjibu maombi namba tatu ambaye ni Makonda, hakuweza kufika mahakamani. Sababu tumemtafuta sana tumeshindwa kumpata tunakusudia kuiomba mahakama tupewe summons mpya,” amedai Wakili Mwasipu.

 

Wakili Mwasipu amedai kuwa, wito huo endapo utatolewa, wanatarajia kuutangaza katika magazeti na kwenye njia nyingine, ili taarifa zimfikie Makonda.

“Tunakusudia kuiomba mahakama hiyo tupewe summons mpya kum-save, ikiwemo kuandika kwenye gazeti na sehemu nyingine yeyote tutakayoona inafaa. Ili aweze kupata taarifa kwamba kuna kesi iko mahakamani,” amedai Wakili Mwasipu.

 

Hii ni mara ya pili kwa Makonda kutohudhuria katika usikilizwaji wa kesi hiyo, ambapo mara ya kwanza alishindwa kuhudhuria tarehe 3 Desemba 2021 bila ya kutoa taarifa yeyote.

Aidha, Wakili Mwasipu amesema kesi hiyo iliyokuwa inatajwa leo, imeahirishwa baada ya Hakimu Lyamuya kuwa na udhuru.

 

“Sababu ya kesi kuahirishwa ni waheshimiwa mahakkimu wanakwenda Segerea kuna shughuli ya kimahakama,” amesema Wakili Mwasipu.

Katika kesi hiyo, Kubenea anamshtaki Makonda kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ikiwemo tukio la uvamizi la ofisi za Kituo cha Televisheni cha Clouds Tv, jijini Dar es Salaam, lkililotokea Machi 2017.

CREDIT: Mwanahalisi

Leave A Reply