Prof. Kabudi Akabidhiwa Uenyekiti Baraza la Mawaziri SADC – (Video + Picha)

Naibu Waziri Mkuu wa Namibia na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Netumbo Nandi- Naitwah akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC unaondelea jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ambapo Tanzania ni mwenyeji wa Mkutano huo wa 39.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amekabidhiwa uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa jumuiya hiyo na Naibu Waziri Mkuu wa Namibia na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Netumbo Nandi- Naitwah aliyemaliza muda wake ikiwa ni sehemu ya mkutano huo utakaohitimishwa na wakuu wa nchi wanachama Agosti 17 na 18, 2019.

 

 

Prof. Kabudi (kushoto) akipokea ngao ikiwa ni ishara ya kuupokea uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

 

 

 

 

Prof. Kabudi akitoa hotuba yake mara baada ya kukabidhiwa uenyekiti huo leo.

 

 

Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakiwa katika mkutano huo.

 

 

 

Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakiwa katika picha ya pamoja.

 

 

 

 


Loading...

Toa comment