The House of Favourite Newspapers

Prof. Lipumba: CUF Hatutashiriki Tena Uchaguzi

0

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimemesema kuwa kutokana na uchaguzi mkuu ulivyoendeshwa nchini, hakubaliani na matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 28, kwa kuwa umegubikwa na mapungufu na kwamba chama hicho hakitashiriki tena uchaguzi wowote na badala yake kitajikita katika harakati za kudai katiba mpya, ili kupatikana kwa tume huru ya uchaguzi.

 

Hayo yamesemwa leo Jumatatu, Novemba 2, 2020 na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba, wakati akizunzgumza na wanahabari jijini Dar es Salaam na kwamba wanafanya hivyo ili kupata tume huru ya uchaguzi.

 

““CUF tunawaomba watanzania wote wapenda haki kuungana na sisi katika ibada siku ya Alhamisi, tutafunga kwa kutokula mchana na tufanye dua na maombi kila mmoja kwa imani yake ili kuomba hukumu ya haki kutokana na kile kilichofanyika kwenye uchaguzi mkuu wa 2020,” amesema Prof. Lipumba .

“Zoezi la kuwaapisha mawakala liliendeshwa kinyume Cha taratibu,Uchaguzi wa Mwaka huu haukuwa na siri. kwa sababu kwenye karatasi za kupiga kura ziko namba za vitambulisho vya wapiga kura,” amesema Lipumba na kuongeza kuwa CUF itaaanzisha mazungumzo na Jumuiya ya Kimataifa kuhusiana na suala hili.

Leave A Reply