The House of Favourite Newspapers

Ndalichako : Elimu ya Watu Wazima Ipewe Kipaumbele

0

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, ametoa wito kwa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kutoa kipaumbele kwa elimu ya watu wazima ili kusaidia katika kuiboresha na kuinua.

 

Prof. Ndalichako ametoa ombi hilo katika Kongamano la kimataifa kuadhimisha miaka 50 ya elimu ya watu wazima Tanzania leo Juni 9, ambapo amesema elimu ya watu wazima ni muhimu kwa nchi yetu.

 

“Kila Halmashauri tunakuwa na afisa elimu ya watu wazima, kuna baadhi ya maeneo elimu ya watu wazima imelala, kila mmoja ajitathimini katika halmashauri yake wanafanya nini na wanamipango gani kuhusu elimu ya watu wazima, naomba TAMISEMI katika mambo yote ya kipaumbele hebu twende na elimu ya watu wazima,” amesema Prof. Ndalichako.

 

Aidha, Prof. Ndalichako amesema kuwa wataandika pendekezo kwa Waziri Mkuu kuhusu maafisa elimu ya watu wazima ambao hawafanyikazi.

 

“Tunapopokea taarifa, tupate pia na taarifa ya elimu ya watu wazima, vinginevyo Waziri Mkuu tutaandika pendekezo maafisa elimu ya watu wazima ambao hawafanyi kazi tuwagawe bure katika maeneo mengine yanayohitaji watu wachapakazi,” amesema Waziri Ndalichako.

Leave A Reply