The House of Favourite Newspapers

Q Chief Amwangukia Diamond “Nisamehe, ni Hasira tu” – Video

0

Msanii nyota wa muziki nchini Tanznaia, amewaomba radhi mashabiki na wadau wa muziki nchini Tanzania kwa kutoa lugha chafu dhidi ya msanii mwenzake, ‘Diamond Platnumz’ na meneja wa nyota huyo mmiliki wa lebo ya WCB Wasafi, Sallam Sharaf ‘#SallamSK.

 

 

Chief ambaye jina lake kamili ni Abubakar Katwila aliomba radhi mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya mwanzoni mwa Februari 2021 video zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii Q Chief akionekana kutoa lugha chafu dhidi ya wawili hao.

 

 

Katika video hiyo, Q Chief pia alisikika akitoa tuhuma za kutumika kwa picha yake kwenye bango linaloonyesha orodha ya wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha la Wasafi Tumewasha iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Januari 31, 2021.

 

 

Alilalamika kuwa licha ya picha yake kuonekana hakuwa akilifahamu uhusika kwake kwenye tamasha hilo na wala hakualikwa.

 

 

Akizungumza na waandishi wa habari Februari 27, 2021, msanii huyo amesema alichukizwa na jambo hilo na hasira ndio zilimfanya kutoa lugha chafu mtandaoni.

 

Hata hivyo, Q Chief amesisitiza kuwa kuomba radhi haimaanishi ameacha kufuatilia jambo hilo.

 

Leave A Reply