Queen Darleen: Naumia Kuishi Bila Mpenzi

Na ALLY KATAMBULA| GAZETI LA AMANI| SHOWBIZ XTRA

MWANAMUZIKI anayefanya vizuri akiwa chini ya Lebo ya ‘WCB’, ‘Queen Darleen’ amefunguka kuwa anaumizwa sana na hali ya kuishi bila mpenzi jambo ambalo limekuwa likimuumiza sana katika maisha yake ya sasa maana yeye pia anahitaji kupenda na kupendwa kama walivyo watu wengine.

Queen Darleen

Akichonga na Showbiz Xtra, Queen Darleen alisema kuwa, tangu aachane na mzazi mwenziye aliyezaa naye mtoto mmoja wa kike hajawahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi jambo ambalo amekuwa akijiuliza bila kupata jibu kuwa linasababishwa na nini.

“Naumizwa na hii hali, kuna wakati huwa nafikiria wanaume wananiogopa au sijui ni kitu gani kinatokea sasa nahitaji kuwa na mpenzi,” alisema Darleen.

Toa comment