The House of Favourite Newspapers

Queen Suzy Adai G-Seven ni Mumewe

Queen Suzy.

Na  GLADNESS MALLYA| RISASI MCHANGANYIKO| ZA MOTOMOTO NEWS

MWANAMUZIKI wa Kundi la FM Academia, Suzan Chubwa maarufu kama Queen Suzy, amedai G-Seven ni mumewe kisheria, kwani ameishi naye zaidi ya miezi sita wakipika na kupakua huku wakijaaliwa mtoto mmoja.

Alisema wameishi kinyumba kwa muda mrefu, kwani sheria za serikali zinasema wawili wanapoishi pamoja kwa miezi sita, wanahesabika kama tayari ni mume na mke, hivyo kwao ndivyo ilivyo na kwamba bado hawajafunga ndoa kanisani, kwani jambo hilo halitaki haraka.

Queen Suzy.

“Ndoa haina haraka kwa sababu kuolewa ni sheria kuzaa ni majaliwa, maadam Mungu ameshatujalia mtoto, hakuna shida akipenda tutafunga tu, harakaharaka haina baraka, ila kiserikali tayari G-Seven ni mume wangu na hata ikitokea tukaachana, mali tuliyonayo tutagawana,” alisema.

Comments are closed.