The House of Favourite Newspapers

R.O.M.A, Nature Kulihamisha Jiji Dar Live!

 


Mwandishi Wetu | Dar es Salaam

WAKALI wasioshikika katika Muziki wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Musa ‘R.O.M.A Mka­toliki’ pamoja na Juma Kassim ‘Nature’ wanatarajiwa kuli­vuta Jiji la Dar Sikukuu ya Pasaka ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uli­opo Mbagala-Zakhem.

Juma Kassim ‘Nature’

Akizungumza na Championi Juma­tano, Meneja na Mratibu wa Dar Live, Juma Mbizo al­isema kuwa, mashabiki wengi wame­kuwa na hamu ya kushudia wakali hao wakipanda juk­waa moja na kulisi­mamisha kama wa­fanyavyo kwenye matamasha mengine.

Ibrahim Musa ‘R.O.M.A Mka­toliki’

“Tumesikia kilio cha mashabiki na tu­mewafikia, R.O.M.A usiku huo atatoa shoo ya mperampera kwa kugonga nyimbo zake zote kali kuanzia Tan­zania hadi K wakati Nature akiwa na TMK Wanaume Halisi watawaonesha mashabiki staili yao mpya huku wak­ilichekecha jukwaa kwa vibao vikali kuanzia Mgambo, Inaniuma Sana hadi Mtumba,” alisema Mbizo.

Mbizo alionge­za kuwa mbali na wakali hao, mapema kuanzia asub­uhi kutakuwa na burudani na michezo mingi kwa watot o itakayoon­gozwa na Kundi la Ma­khirikhiri kutoka Tanzania.

“Pia tutakuwa na msanii gumzo kila kona, Harmorapa wakali wa Singe­li, Dulla Makabila na Msaga Sumu na wengine wengi,” alisema Mbizo.

 

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe nisiasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaa, muziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.

Comments are closed.