The House of Favourite Newspapers

Rachel Siwezi Ku-date na Msanii

0

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Winifrida Joseph ‘Rachel’ amesema katika maisha yake, hajawahi na wala hatarajii kutoka kimapenzi na msanii, kwa sababu ana wivu usio wa kawaida.

Akizungumza na AMANI, Rachel ambaye anadaiwa kuwa na swaga za Ray C, amesema wasanii wengi hukutana na vishawishi jambo ambalo linazidisha wivu katika mahusiano.

“Ukiwa na uhusiano, jiandae kupata presha au kufa kabisa, ndiyo maana siwezi kabisa kuwa na uhusiano na msanii… kwa sababu anaweza akafanya video na mdada mwenye sifa zote ukiangalia sura anayo, shepu ndiyo usiseme, cha kufa na presha ni kitu gani? Wala siwataki,” alisema Rachel.

 

Stori: Khadija Bakari

Leave A Reply