The House of Favourite Newspapers

Raia wa Uganda Waishataki Kampuni ya TotalEnergies ya Ufaransa mjini Paris

0

Raia 26 wa Uganda wameishtaki kampuni kubwa ya mafuta ya Ufaransa ya TotalEnergies mjini Paris wakida fidia kwa madai ya ukiukaji wa haki za binadamu katika miradi yake mikubwa nchini humo, huku waandamanaji wa hali ya hewa wakilenga makao makuu ya kampuni hiyo iliyopo Uingereza.

Wakiungana na makundi matano ya misaada kutoka Uganda na Ufaransa, watu kutoka jamii zilizoathirika wanasema kampuni ya nishati ilisababisha “madhara makubwa”, hasa kwa haki zao za ardhi na chakula.

“Tunachoomba mahakama itambue wajibu wa kampuni hiyo kwa raia na iihukumu kampuni hiyo kuwalipa fidia watu walioathirika” alisema Juliette Renaud msemaji wa shirika la mazingira la Friends of the Earth la Ufaransa.

Kiini cha malalamiko yao waliyofikisha katika mahakama ya Paris yanahusu miradi miwili mikubwa ya TotalEnergies: utafiti wa Tilenga wa visima 419 vya mafuta, ambapo theluthi moja ya visima hivyo vipo katika eneo la Murchison Falls ambalo ni mbuga kubwa ya kitaifa ya Uganda. Wakati bomba la EACOP lenye urefu wa kilomita 1,500 la kusafirisha mafuta ghafi kwenda pwani ya Tanzania kupitia hifadhi kadhaa za asili.

EACOP pia ililengwa siku ya Jumanne na wanaharakati wa hali ya hewa wa London ambao walipuliza rangi kwenye ukumbi wa makao makuu ya kampuni hiyo ya TotalEnergies yaliyoko Uingereza katika wilaya Canary Wharf.

TotalEnergies ilisema katika taarifa yake kwamba “inaheshimu kikamilifu haki za msingi za uhuru wa kujieleza, lakini inachukia aina zote za vurugu, iwe za maneno, kimwili au kutumia nyenzo”.
watu walioko katika maeneo hayo,walioathiriwa na shughuli hizo “wamezuiliwa kuitumia ardhi yao kwa miaka mitatu au minne, kinyume na haki zao za kumiliki aridhi”, vyama wanaharakati vilivyopo Ufaransa na Uganda vilisema katika taarifa.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters.

MUSUKUMA AWACHANA SIMBA “WANASAJILI MAKAPI, MPIRA NI PESA SIO SWAGA MPIRA UNAHITAJI PESA”

Leave A Reply