The House of Favourite Newspapers

Rais Magufuli Akizindua Ujenzi wa Reli ya Kimataifa Dar-Moro

0

RAIS Dkt John Pombe Magufuli amezindua Rasmi ujenzi wa Mradi wa Reli ya Kisasa ya Kimataifa ambayo treni ya kisasa inayotumia umeme itaweza kusafiri kwa mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Mkurugenzi wa RAHCO alianza  kwa kueleza;

“Reli ya kisasa itakayojengwa, treni itaweza kusafiri kwa KM 160/saa, na itatumia umeme na mafuta. Treni itaweza kutoka Dar kwenda Dodoma kwa saa 2 na dakika 50, Dar – Mwanza kwa saa 7 na dakika 40.

“Treni itakuwa na urefu wa Km 2, sawa na semitrailer 500 na itakuwa na mabehewa 100. Iwapo dereva atakiuka taratibu, muongozaji aliyeko Dar anaweza kuizima treni hata kama ipo Mwanza.

“Kutajengwa mifumo ya mawasiliano na ya mizigo njiani, itaweza kubeba tani milioni 15 kwa mwaka. Ujenzi wa Reli hiyo utafanyika kwa muda wa miezi 30 hadi kukamilika.

“Ujenzi wa Reli hiyo utagharimu dola bilioni 1.29 bila kodi na dola bilioni 1.8 pamoja na kodi. Sehemu za milima patajengwa madaraja ili treni iweze kupita kirahisi. Treni itaweza kutoka Dar kwenda Dodoma kwa saa 2 na dakika 50, Dar – Mwanza kwa saa 7 na dakika 40.

Rais Magufuli amemtaka mkandarasi wa mradi huo kuhakikisha kuwa ikiwezekana anaumaliza mradi kabla ya miezi 30 ili wananchi waondokane na adha ya usafiri.

Aidha Rais ameongeza kuwa ni Tanzania pekee kwa nchi zote za Afrika ambayo imeweza kujenga mradi wa reli kama huo kwa pesa zake za ndani.

Rais Magufuli pia ameagiza ujenzi wa Reli hiyo ya kisasa ya Dar-Morogoro utakapoanza, ajira zote wapewe wakazi wa Pugu.

FUATILIA TUKIO ZIMALA UZINDUZI

Leave A Reply