The House of Favourite Newspapers

Rais Magufuli Amjulia Hali Mzee Mwinyi Aliyelazwa – Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea kumjulia hali Jijini Dar es Salaam, leo Disemba 5,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, leo Desemba 5, 2018, amemtembelea na kumjulia hali Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi Jijini Dar es Salaam.

 

Rais Magufuli wakiomba Dua Maalumu na Rais Mstaafu, mzee Mwinyi, Bi. Sitti Mwinyi (Mke wa Mzee Mwinyi) pamoja na Abdallah Mwinyi (Mtoto wa Mzee Mwinyi) alipomtembelea kumjulia hali leo.

Pamoja na Kumjulia hali, Rais Dkt. John Magufuli ameshiriki dua ya kumuombea Afya Njema iliyoongozwa na familia ya Rais huyo mstaafu.

 

Rais Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu Mwinyi alipomtembelea kumjulia hali.

Walioshiriki wa Dua hiyo Maalumu ni Rais Magufuli mwenyewe, Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Bi. Sitti Mwinyi (Mke wa Mzee Mwinyi) pamoja na Abdallah Mwinyi (Mtoto wa Mzee Mwinyi).

 

Rais Magufuli akiagana na Bi Sitti Mwinyi. (PICHA NA IKULU).

Rais Magufuli ameiaga familia hiyo kwa kuwapa moyo kuwa mzee Mwinyi atarejea kwenye hali yake ya kawaida na kikubwa waendelee kumuombea tu.

 

Taarifa zaidi bado hazijaelezwa kuwa ni ugonjwa gani unamsumbua Rais Mwinyi na amelazwa katika hospitali gani.

BREAKING: Mwinyi Alazwa Rais Magufuli Amuombea Dua

Comments are closed.