The House of Favourite Newspapers

RAIS MAGUFULI AONGOZA MAMIA CHATO MAZISHI YA DADA YAKE (VIDEO +PICHA)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mama yake mzazi Suzana Magufuli wakati wakitoa heshma za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.

MWILI wa Dada wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Marehemu Monica Magufuli umezikwa nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita leo Jumanne, Agosti 21, 2018.

Rais Magufuli akitoa heshma za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.

Viongozi mbalimbali wa serikali, siasa na dini wakiwemo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Marais wastaafu, Ally Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, mkewe, Bi. Mary Majaliwa, wabunge, Mama Salma Kikwete, RC Paul Makonda na wengine wameungana na familia ya Magufuli katika kumsindikiza Monica kwenye nyumba yake ya milele.

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete akitoa heshma za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Monica Magufuli.

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Mkewe Mama Marry Majaliwa wakitoa heshma zao za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Monica Magufuli katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.

Bi. Monica alifariki dunia Jumamosi iliyopita, Hospitali ya Bugando alikokuwa amelazwa akipatiwa matuibabu.

Baba Askofu mkuu Mwandamizi Yuda Thaddeus Ruwaichi akiongoza Misa ya kumuombea Marehemu Monica Magufuli Chato mkoani Geita
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsaidia Mama yake mzazi Suzana Magufuli wakati wakuweka udongo ndani ya kaburi la Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka udongo ndani ya kaburi la Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.

Comments are closed.