The House of Favourite Newspapers

Rais Magufuli Azindua Ikulu Mpya, Chamwino – Dodoma

Rais John Magufuli  leo amesema dhamira yake ya kuhamia Dodoma iko pale pale ila amechelewa kufanya hivyo kwa sababu ya kuuguliwa na mama yake.

“Waziri Mkuu na Makamu wa Rais wameshahamia hata mimi nakuja, nilichelewa kuhamia Dodoma kwa sababu ya kuuguliwa na mama yangu ambaye hadi sasa yupo hospitali ila nawahakikishia nakuja na hakuna kitu kingine cha kunichelewesha,” amesema.

Mapema leo asubuhi Rais Magufuli alifungua ofisi ya Rais iliyojengwa eneo la Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Comments are closed.