The House of Favourite Newspapers

Rais Magufuli: Mambo Haya Wabunge Hawapendi Niyaseme – VIDEO

RAIS Dkt. John Magufuli amewataka wabunge kutumia fedha za mfuko wa jimbo, kutatua baadhi ya changamoto katika majimbo yao ikiwemo ujenzi wa miradi ya maendeleo badala ya kusubiri serikali kuu ifanye kila kitu.

 

Magufuli ameyasema hayo leo Mei 2, 2018 wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi, katika Hospitali ya wilaya ya Kilolo mkoani Iringa na kuongeza kuwa baadhi ya changamoto zinaweza kutatuliwa kwa kutumia fedha za mfuko wa jimbo hilo.

 

“Miradi yote si lazima ifanywe na Serikali Kuu, wewe Mbunge unafedha za jimbo na haya wabunge hawapendagi niseme, ukichukua milioni 5 au 10 ukanunua mota, ukaunga bomba, mota itayavuta maji kuyapeleka katika kijiji kingine utakuwa umesaidia, si lazima uchimbe kisima. Halmashauri zisikwepe majukumu yake, posho za madiwani wamehudhuria vikao/semina siku 2 unaandika siku 4, badala ya kuziweka fedha hizo na kuzipeleka katika miradi ya maji.

 

“Madiwani ndiyo mnaowakilisha wananchi, nataka mhakikishe fedha zinazoletwa katika halmashauri zinatumika kwa ajili ya maendeleo na siyo katika shughuli nyinginezo tofauti na ilivyopangwa.

Akizungumzia wakulima, Rais amesema;

“Nilishasema, iwapo mzigo una uzito chini ya tani 1, usilipe hata senti 5, ninafahamu wapo watendaji wa halmashauri ambao wanaweza kuwa wanawalipisha ushuru, sasa waambieni na wao waende mashambani ili wakajue uchungu wa ushuru.

“Nataka mfahamu kwamba, wakulima wetu sio chombo cha kuwatajirisha watendaji wa halmashauri, nataka wakurugenzi wote mbandike tozo katika ofisi zenu ili wananchi/wakulima wajue tozo hizo kwaba zimefutwa.

VIDEO: MSIKIE MAGUFULI AKIHUTUBIA

Comments are closed.