The House of Favourite Newspapers

RAIS MAGUFULI NA MKEWE WASHIRIKI MISA PAROKIA YA OYSTERBAY – VIDEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Janeth Magufuli pamoja na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki wakishiriki Misa Takatifu Dominika ya 18 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko Msaidizi Padre Paul Haule, Agosti 04,2019.
Rais  Magufuli akiwa na mkewe Janeth Magufuli pamoja na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki wakishiriki Misa Takatifu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Janeth Magufuli wakipeana mkono wa Amani na Waumini wengine wakati wa Misa.
Rais  Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Simon Sirro nje ya kanisa  baada ya Misa Takatifu.
Rais wa Magufuli akisaliana na muumini na mtoto wake mara baada ya Misa.
Rais Magufuli akimnunulia muumini Rosari baada ya Misa Takatifu ya Dominika ya 18 ya Mwaka “C” .

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Janeth Magufuli leo Jumapili, Agosti 8, 2019 wameungana na Waumini wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam kushiriki Misa Takatifu Dominika ya 18 ya Mwaka “C.

Comments are closed.