The House of Favourite Newspapers

Rais Mnangagwa Amaliza Ziara Yake Nchini – Pichaz

Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe, Emmerson Dambudzo Mnangagwa amemaliza ziara yake rasmi ya kiserikali ya siku mbili nchini Tanzania leo Ijumaa, Juni 29, 2018.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam ameagwa na mwenyeji wake, Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa aliwasili Tanzania jana na kukubaliana na Rais John Magufuli kushirikiana kibiashara, utalii na kijamii huku akisema shambulio lililofanywa dhidi yake Juni 23, katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika mjini Bulawayo nchi humo akisema lilikuwa dogo na nchi yake iko salama.
Mambo Matatu Waliyokubaliana
Kukuza uwekezaji, nimemwambia kuna hekta 44 milioni za ardhi inayofaa kwa kilimo na kuna hekta 29 milioni zinazofaa kwa umwagiliaji. Vilevile kuna uwekezaji wa mifugo, uvuvi na uchakataji wa madini.
Kushirikiana wakitumia wingi wa vivutio vilivyopo nchini ili kuwavutia na kutumia mikataba ya mashirika ya ndege likiwamo la Fasjet, mtalii akitoka Victoria Falls aende pia Serengeti halafu amalizie safari yake kwenye fukwe nzuri za Zanzibar.
Ushirikiano katika huduma za jamii ikiwamo elimu, afya na utamaduni na hasa katika lugha ya Kiswahili ambayo alisema Tanzania ina walimu wa kutosha.

MNANGAGWA ALIVYOWASILI NCHINI JANA

Comments are closed.