The House of Favourite Newspapers

Mwinyi Amwapisha Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi leo Januari 2, 2021, amemwapisha Mhandisi Zena Ahmed Said kuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, tukio lililofanyika katika Ikulu ya Zanzibar.

Mhandisi Zena ambaye anakuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, anachukua nafasi ya Abdulhamid Yahya Mzee ambaye amemaliza utumishi wake serikalini na kustaafu.

Leave A Reply