The House of Favourite Newspapers

Waliokufa kwa Corona Kuchomwa Moto

0

KIONGOZI  wa Baraza la Waislamu wa Sri Lanka Mbunge,  Rauff Hakim, alisema kuwa uteketezaji wa miili ya wahanga wa janga la corona (Covid-19) unaleta hisia za kuwatenga watu walio katika jumuia za wachache nchini Sri Lanka.

 

Rauff Hakim alisema hayo wakati akitathmini zoezi la serikali ya Sri Lanka la kuchoma moto miili ya watu waliokufa kutokana na Covid-19 kwenye chumba cha maiti, huku akitoa sababu za kiafya. Alisema uamuzi uliotekelezwa tangu Machi 2020 ni wa kisiasa.

 

“Zoezi hili ni mwendelezo wa mradi wa kuchochea chuki za Waislamu walio wachache nchini. Hatua hii ilianza baada ya shambulizi la kanisa la mwaka 2019. Shambulizi lilikuwa chanzo muhimu sana kwa kutekeleza lengo la kisiasa la serikali la kuteketeza miili ya Waislamu,” alisema.

 

Hakim alibainisha kuwa serikali ilikuwa ikijaribu kuleta hofu kwa Waislamu kwa kutumia njia ya kuteketeza miili yao bila kuzingatia msingi ya kisayansi na kuongeza:

 

“Uteketezaji wa lazima wa waathiriwa wa Covid-19 unawatenga watu wachache wa Sri Lanka na pia unasababisha uharibifu mkubwa wa kijamii.”

 

Hanaa Singer ambaye ni Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN) mjini Colombo, alimtaka Waziri Mkuu wa Sri Lanka ,Mahinda Rajapaksa, “kuyachunguza kiundani maamuzi kama haya yanayohusu janga la Covid-19” katika ujumbe wake.

 

Leave A Reply