The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Aagiza Tafiti za Saratani

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameagiza kufanyika kwa utafiti wa kina kuhusu ongezeko la wagonjwa wa saratani katika ukanda wa ziwa victoria kwa kusema kuwa takwimu za sasa zinatishia usalama wa afya za wananchi wa maeneo hayo.

 

Ametoa agizo hilo wakati akihutubia katika maadhimisho ya jubilee ya miaka 50 ya hospitali ya Bugando jijini Mwanza, mapema Novemba 18, 2021.

 

Rais Samia afikia maamuzi hayo kufuatia kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa kutoka wagonjwa 1200 mwaka 2019 hadi 1500 kwa mwaka huu wa 2021, takwimu hizo zinaonesha kuwa wagonjwa wengi ni wanawake na wanaugua hasa saratani ya shingo ya kizazi.

 

“Nielekeze umuhimu wa tafiti kwani ongezeko la wagonjwa wa saratani kwa kanda hii ya ziwa ni kubwa, kinachoniumiza akili ni wagonja wengi ni wanawake” amesema Kiongozi huyo Mkuu wa Nchi.

 

Amesisitiza kufanyika kwa tafiti hizo kufuatia kuwepo kwa madai mengi kuwa ongezeko la idadi hiyo linasababishwa na matumizi ya maji yenye kemikali za zebaki zinazopatikana katika migodi ya madini.

 

“Wanasema kuwa sababu ni maji yanayotumika kuwa yana mabaki ya Zebaki yanaathiri mwenendo wa afya ya mwanadamu na kwa ukubwa yanawaumiza akina mama, niagize utafiti wa kina,” amesema Rais Samia.

 

Leave A Reply