The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Avunja Ukimya Sakata la Mgao wa Maji Dar – Video

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametoa ufafanuzi wa adha inayoikumba taifa jumla kwa sasa ya kukatika kwa maji na umeme kwa kusema kuwa shida hizo ni za muda mfupi kwani serikali imeingia kazini kumaliza tatizo hilo.

 

Akihutubia kaika maadhimisho ya jubilee ya miaka 50 ya hospitali ya Bugando iliyopo jijini Mwanza leo Novemba 18, 2021 amesema adha hii imesababishwa kwa kiasi kikubwa na sababu ambazo nyingi ni za kibinadamu ambazo kimsingi zimefanyika kwa makusudi.

 

Amezitaja sababu hizo kuwa ni Ubishi na ukaidi wa baadhi ya watu pamoja na Kudra ama mipango ya Mwenyezi Mungu.

 

Akifafanunua kuhusu ubishi na ukaidi, Rais Samia amesema kuwa, wapo watu waliovamia maeneo ya vyanzo vya maji ambao wengi wao ni wakulima na wafugaji.

 

Amesema kuwa wapo wakulima walioweka kambi katika bonde la mto Ruvu juu na chini kisha kuziba mtiririko wa maji wa kawaida hivyo kupelekea kushuka kwa kima cha maji katika bonde hilo.

 

“Dar es Salaam ina shida ya maji kubwa sana, tumekuta magogo, blocks yamewekwa huko ili kuzuia maji yasitiririke kawaida, huu ni uhujumu wa makusudi.

 

“Kwenye bonde la mto Ruvu na Ruaha kuna wafugaji wamehamia huko wanalisha na kunyweshwa maelfu ya mifugo, fikirieni ng’ombe mmoja anakunywa lita 40 za maji vipi kuhusu maelfu ya ng’ombe, tutapata wapi maji? Amesema Rais Samia.

 

Amezitaja sababu nyingine zinazoababisha kupungua kwa maji kuwa ni pamoja na vitendo vya ukataji na uchomaji wa misitu, mabadiliko ya tabianchi pamoja na mipango ya Mungu.

 

Ameongeza kusema kuwa Serikali haitawafumbia macho wale wote wanaohujumu miundombinu ya vyanzo vya maji kwa manufaa yao wenyewe.

 

Leave A Reply