The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Afanya Uteuzi VETA na Kamishna wa Petroli na Gesi Nchini

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua CPA Anthony Mzee Kasore kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA). Kabla ya uteuzi huu, CPA Kasore alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Aidha Dkt. Samia amemteua Bw. Goodluck Antipas Shirima kuwa Kamishna wa Petroli na Gesi, Wizara ya Nishati. Bw. Shirima ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Uhusiano Kampuni ya Mafuta ya Puma, Tanzania.

Leave A Reply