The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Akishiriki Misa Maalum Ya Miaka 40 Ya Kumbukizi Ya Kifo Cha Hayati Sokoine (Picha +Video)

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza mara baada ya Ibada Maalum ya Kumbukizi ya miaka 40 tangu kutokea kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine. Ibada hiyo ya Misa Takatifu imefanyika nyumbani kwa Hayati Sokoine Monduli Mkoani Arusha tarehe 12 Aprili, 2024.
Rais Samia akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine Monduli Mkoani Arusha tarehe 12 Aprili, 2024.
Rais Samia  akiteta jambo na Mama Fatma Karume Mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume ambaye pia alihudhuria Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya miaka 40 tangu kutokea kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine.
Matukio mbalimbali katika Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya miaka 40 tangu kutokea kifo cha Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine. Ibada hiyo imefanyika nyumbani kwa Hayati Sokoine Monduli Mkoani Arusha tarehe 12 Aprili, 2024.
Rais Samia akiteta jambo na Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo aliyehudhuria pia Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya miaka 40 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wakati wa Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya miaka 40 tangu kutokea kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine. Ibada hiyo imefanyika nyumbani kwa Hayati Sokoine Monduli Mkoani Arusha tarehe 12 Aprili, 2024.
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya miaka 40 tangu kutokea kifo cha Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine.
Baadhi ya Wenza wa Viongozi wakiwa kwenye Ibada.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria Ibada ya Misa Takatifu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akishiriki Misa Maalum ya miaka 40 ya Kumbukumbu ya Miaka 40 ya kifo cha Hayati Edward Moringe Sokoine, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Nyumbani kwa Hayati Sokoine Monduli Juu, Mkoani Arusha tarehe 12 Aprili, 2024

Hayati Edward Moringe Sokoine alifariki tarehe 14 Aprili, 1984 ambaye sasa imetimia miaka 40 ya kifo chake.

Mbunge wa Jimbo la Monduli, Fred Edward Lowasa ameungana na Wageni na viongozi mbalimbali kushiriki Ibada Maalum ya Kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya kwanza, Hayati Edward Moringe Sokoine, inayofanyika nyumbani kwake Kijiji cha Enguik, Kata ya Monduli Juu, wilaya ya Monduli leo 12, Aprili, 2024.
Mama Regina Lowassa ameungana na Wageni na viongozi mbalimbali.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb) na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Rizwan Kikwete (Mb), wakizungumza mara baada ya kuwasili Monduli Juu, kushiriki Ibada Maalum ya Kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya kwanza, Hayati Edward Moringe Sokoine,
Wageni na viongozi mbalimbali Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Abdulrahaman Kinana, akizungumza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb) (kushoto) na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Mosses Nnauye (kulia)
Askofu wa Kanisa la Rise & Shine Boniface Mwamposa ameungana na wagene na viongozi mbalimbali wa dini, chama na Serikali, kushiriki Ibada Maalum ya Kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya kwanza, Hayati Edward Moringe Sokine, inayofanyika nyumbani kwake Kijiji cha Enguik, Kata ya Monduli Juu, wilaya ya Monduli leo 12, Aprili, 2024.

Leave A Reply