The House of Favourite Newspapers

Rais Samia alivyowasili uwanja wa Ndege wa Ankara Esenboga Uturuki kwa ajili ya Ziara

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ankara Esenboga nchini Uturuki kwa ajili ya Ziara Rasmi tarehe 17 Aprili, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Dkt Samia Suluhu Hassan yupo nchini Uturuki kwa ajili ya Ziara Rasmi tarehe 17 hadi 21 Aprili 2024.
Ziara inafanyika kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan viongozi hao watashuhudia kusainiwa kwa Hati za Makubaliano nane (8) katika sekta za Elimu, Utalii, Utunzaji Kumbukumbu na ushirikiano katika masuala ya Diaspora.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ankara Esenboga nchini Uturuki kwa ajili ya Ziara Rasmi tarehe 17 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Waziri wa Familia na Huduma za Jamii wa Uturuki Mahinur Ozdemir Goktas mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ankara Esenboga nchini Uturuki kwa ajili ya Ziara Rasmi tarehe 17 Aprili, 2024.
Leave A Reply