The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Alivyozindua Tawi la Benki ya PBZ na NMB Paje Zanzibar – Picha

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Tawi la Benki ya NMB Paje katika shamrashamra za Tamasha la Kizimkazi (Usiku wa Samia) Paje, Zanzibar tarehe 30 Agosti, 2023.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, jana amezindua Tawi la Benki ya NMB Paje, Mkoa wa Kusini Unguja, hapa Zanzibar, uzinduzi unaoendelea kupanua mtandao wa matawi ya benki hiyo nchini na kufikia 230, yanayohudumia zaidi ya Wateja Milioni 6.

Uzinduzi huo ambao ni sehemu ya Tamasha la Kizimkazi (Kizimkazi Festival 2023), ulioweka rekodi ya mahudhurio makubwa ya viongozi waandamizi wa Serikali na wastaafu, umekuja siku 58 tangu Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango alipozindua tawi la 229 la Benki ya NMB Buhigwe mkoani Kigoma.

Rekodi ya mahudhurio makubwa ya viongozi waandamizi wa Serikali imewekwa katika uzinduzi wa NMB Paje, ambako ukiondoa Rais Samia, wengine waliohudhuria ni pamoja Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Gavana Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba na Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba.

Viongozi wengine ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa, Katibu Mkuu Kiongozi na Balozi Moses Kusiluka.

Rais Samia aliwasili tawini NMB Paje majira ya saa 10:15 alasiri na ilimchukua dakika chache Bi Zaipuna kumpa maelezo mafupi ya tawi hilo na NMB kwa ujumla, ambako alimweleza kuwa tawi hilo linaenda kumaliza changamoto ya wakazi wa Paje kusafiri umbali wa kilomita 60 kufuata huduma zetu za kibenki kwenye Tawi la Mwanakwerekwe.

Baada ya maelezo hayo, Mheshimiwa Rais alikata utepe kuashiria ufunguzi wa tawi hilo, kabla ya kuingia ndani kukagua miundombinu na Mifumo ya utoaji huduma ndani ya jengo hilo.

Akiwa ndani ya tawi, Rais Samia alitembezwa katika Ofisi za Vitengo na Idara mbalimbali, zoezi lililofanyika kwa dakika 15, kabla ya kuondoka hapo na kuingia kwenye Viwanja vya Paje, vilivyopo mita 50 tu kutoka hapo, alikozungumza na wananchi wakati wa kuubariki Usiku wa Samia, ambao ni sehemu ya Kizimkazi Festival.

NMB Paje linakuwa ni tawi la 133 katika kipindi cha karibu miaka 26 ya benki hiyo ambayo ilikuwa na matawi 97 wakati ikianzishwa mwaka 1997. NMB Tawi la Paje linakuwa ni la tatu kufunguliwa na benki hiyo mwaka huu 2023, likitanguliwa na matawi ya Kwa Mrombo jijini Arusha (Mei 3) na Buhigwe Kigoma (Julai 4).

Rais Samia akiwa na viongozi wengine wakati akikata utepe kuzindua Tawi la Benki ya PBZ Paje Zanzibar katika shamrashamra za Tamasha la Kizimkazi (Usiku wa Samia) Paje, Zanzibar tarehe 30 Agosti, 2023.
Rais Samia akizindua Tawi la Benki ya PBZ Paje Zanzibar katika shamrashamra za Tamasha la Kizimkazi .
Rais Samia  akipokea kadi ya ZATO Prepaid Card kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna mara baada ya kuzindua Tawi la Benki hiyo lililopo Paje katika shamrashamra za Tamasha la Kizimkazi (Usiku wa Samia), Zanzibar tarehe 30 Agosti, 2023.
Rais Samia akifurahia jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna mara baada ya kupokea Kadi ya ZATO Prepaid

 

 

Leave A Reply