The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Awaapisha Viongozi Wateule Atoa Maagizo Mazito Ikulu, Dar – Video

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza katika hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Machi, 2024.

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa yeye hana kundi, bali anafanya kazi na kuwaongoza wotanzania wote kwa usawa na ndivyo alivyowataka wakuu wa mikoa wakafanye kazi kwa usawa kama yeye anavyofanya.

Rais Samia ameyasema hayo mara baada ya kuwaapisha baadhi ya viongozi aliyowateua siku chache zilizopita Ikulu jijini Dar es Salaam leo Machi 13, 2024.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Machi, 2024.
Wakuu wa Mikoa ya Songwe, Mtwara, Tabora na Shinyanga, Naibu Katibu Mkuu (Muungano na Mazingira) pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabasi yaendayo Haraka (UDART) wakila Kiapo cha Maadili kwa viongozi wa Umma kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Machi, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Christina Solomon Mndeme kuwa Naibu Katibu Mkuu (Muungano na Mazingira) kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Machi, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Anamringi Macha kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Machi, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Paulo Matiko Chacha kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Machi, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Kanali Patrick Kenan Sawala kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Machi, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Daniel Godfrey Chongolo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Machi, 2024.

Leave A Reply