The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Awasili Kenya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 28 Aprili, 2024. Rais Samia anatarajia kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA. IDA ni Mfuko Maalum wa Benki ya Dunia unaotoa mikopo nafuu na misaada kwa nchi zinazoendelea.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasili Jijini Nairobi nchini Kenya Aprili 28, 2024 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA

Rais Samia  akiteta jambo na Waziri wa Afya wa Kenya Susan Nakhumicha mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi nchini Kenya.
Rais Samia akifurahia jambo na Waziri wa Afya wa Kenya Susan Nakhumicha (kulia) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi nchini Kenya.
Rais Samia akisalimiana na viongozi mbalimbali waliofika kumpokea.
Rais Samia akipokea zawadi ya Ua mara baada ya kupokelewa na Watanzania Waishio Jijini Nairobi.
Rais Samia akiteta jambo na Waziri wa Afya wa Kenya Susan Nakhumicha (kulia).
Rais Samia akifurahia jambo na baadhi ya Watanzania waliofika kumpokea.

WAZIRI SILAA AFIKA GEREZANI KUTATUA MGOGORO WA MIPAKA- ”RAIS SAMIA AMENITUMA NIWAHUDUMIE WANANCHI”

 

Leave A Reply