The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Kufanya Maamuzi Magufmu Wizara ya Afya – Video

0

KATIKA kuboresha huduma ya afya nchini, Serikali imenuia kuitenga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutoka kwenye ujumuishi huo hadi kujitegemea kuwa Wizara ya Afya ili kupambana na majanga yanayoendelea duniani.

 

Haya yameweka wazi na Rais Samia mapema Desemba 16, 2021 wakati akizindua kamati ya ushauri ya kitaifa ya utekelezaji wa ahadi za nchi na kubainisha kuwa Wizara ya Afya ya Tanzania bara na Visiwani inapaswa kuondolewa kwenye vipengele vya maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

 

Amesema sababu ya kuitenga Wizara hiyo ni kufuatia kutotimia kwa malengo mengi yanayowekwa kwenye Wizara hiyo kutokana na mlundikano wa vipengele nyingi ndani ya Wizara moja.

 

“Maamuzi yangu ni kuitenga Wizara itakayoshughulikia Jinsia Maendeleo ya Wanawake kutoka kwenye kuchanganywa na Wizara ya Afya kwa sababu tukiweka Wizara ya Afya na mambo mengine na hali tuliyonayo sasa hivi duniani Sekta ya Afya peke yake inachukua sura kubwa.

 

“Tukiiweka Wizara ya Afya na mambo mengine kama haya na ukiunganisha na yanayoendelea duniani tunakuwa tunaiminya. Lakini kama tutaitenga Wizara hii na mambo haya itaweza kufanya kazi vizuri,” Amesema Rais Samia.

 

Aidha ameongeza kusema kuwa atazungumza suala hilo na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ally Mwinyi ili kuona namna ya kufanikisha adhima hiyo.

 

Leave A Reply